Mwanamke mmoja nchini Kenya, Ann Akiru ameshambuliwa kwa mapanga na mumewe mara baada ya kumnyima unyumba.

John Lokoreno ambaye ni mume wa mwanamke huyo inadaiwa alijiua mara baada ya kufanya shambulio hilo nchini humo.

Aidha, Ann anadai kuwa yeye na mumewe wamekuwa hawaelewani ndani ya familia yao tangu mwezi Februari mwaka huu na alimualika mama yake kusuluhisha hali hiyo. ambapo yeye na mumewe walikubaliana kuondoa tofauti zao na kusonga mbele.

Amesema kuwa baada ya mama yake kuondoka, mwanaume huyo alirudi nyumbani na kumkuta mke wake akiwa anandaa chakula alifunga mlango na kuanza kumshambulia kwa mapanga

Hata hivyo, ameongeza kuwa mume wake alikuwa akimpa vitisho na kumchunguza mara kwa mara kupitia kwa marafiki na ndugu zake.

 

Nandy aomba radhi Kanisa, Serikali kwa video yake ya utupu
Nicki Minaj kushusha vyuma viwili leo, aonjesha kishindo

Comments

comments