Mwanaume mmoja mkazi wa Elkhart Lake, Marekani anakabiliwa na shtaka la kutishia maisha baada ya kumtumia mpenzi wake wa zamani chatu aliye hai akijifanya kuwa ni zawadi ya chakula.

Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Eric Burrows (37) anadaiwa kuwa alikuwa katika mtafaruku mkubwa na mpenzi wake huyo wa zamani ambaye jina lake limehifadhiwa, mtafaruku ambao umedaiwa kushika kasi tangu Julai 30 hadi Agosti 18 mwaka huu.

Jeshi la Polisi limeeza kuwa mwanamke huyo ameeleza kuwa alikuwa anaishi nyumba moja na Burrows lakini walishindwana na ndipo alipoamua kuachana naye na kutafuta nyumba nyingine. Lakini tangu alipohama alijikuta akipokea vitisho vingi kutoka kwa mtu huyo.

Alisema kuwa Burrows alitishia hadi mwajiri wake na siku ya mwisho alituma zawadi ofisini kwake akidanganya jina la mtumaji ili zawadi hiyo ifike na kufunguliwa na mwanamke huyo.

Alisema kuwa baada ya kushtukia, alijaribu kufuatilia kwa wataalam wa mawasiliano sehemu ambayo namba ya mtuma zawadi ilitokea ndipo alipogundua ni eneo ambalo anaishi Burrows.

Mwanamke huyo alisema kuwa waliamua kuu-scan mzigo huo waligundua ulikuwa na chatu ndani yake akiwa hai pamoja na ujumbe uliosomeka, “Surprise you lying b*cth ..Enjoy, this is who you are. Now do you care.”

Mwanaume huyo pia anadaiwa kumtishia maisha mwanaume anayeishi na mwanamke huyo hivi sasa.

Vijana Chini Ya Umri Wa Miaka 17 Wamkuna Kocha Azam FC
Jurgen Klopp: Bado Ninamuhitaji Daniel Sturridge