Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linamtafuta Emmanuel Richard anayedaiwa kumuua mama mkwe wake Maria Batholomeo baada ya kuingilia ugomvi wake na mke wake.

Kamanda wa Polisi wa Manyara, Merrisone Mwakyoma ameeleza hayo wakati akizungumza na Dar24 Media ambapo ameeleza kuwa mnamo Juni 20, 2021 Marehememu Maria Batholomeo alishambuliwa kwa kupigwa na kitu kigumu kifuani ambapo baada ya hapo alipelekwa kituo cha polisi Magugu na baadaye kukimbizwa kituo cha afya Magugu na ndipo umauti ulimkuta.

Inadaiwa awali Emmanuel Richard alimpiga mkewe Theresia Samwel ambaye baada ya kupigwa aliamua kukimbilia kwao na ndipo mama mkwe alipojaribu kusuluhisha ugomvi wa wawili hao.

Kamanda Mwakyoma ametoa rai kwa wanandoa na watu wengine inapotokea mtu anapigwa kukimbilia kituo cha polisi kwa ajili ya usalama kuliko kukimbilia nyumbani.

Mwanzilishi wa Antivirus ya McAfee afariki dunia
Yanga, TFF mambo safi