Mwanamke mmoja raia wa Morocco anatuhumiwa kumuua mpenzi wake na kumfanya kitoweo huko Falme za Kiarabu.

Tukio hilo linadaiwa kufanyika miezi mitatu iliyopita, lakini limegundulika hivi karibun baada ya jino la binaadamu kuonekana kwenye mashine ya kusagia matunda ya mwanamke huyo.

Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo, na kusema ulikuwa ni wakati wa “uendawazimu”, gazeti la serikali la The National limeripoti.

Aidha, Mwanamke huyo ambaye anakadiliwa kuwa na umri wa miaka 30 atapandishwa kizimbani baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

Wapenzi hao walikuwa katika mahusiano kwa miaka saba. kwa mujibu wa The National, mwanamke huyo alimuua mpenzi wake baada ya kumwambia kuwa alikuwa anapanga kumuoa mwanamke mwingine.

Hata hivyo, polisi hawajaeleza ni namna gani mauaji hayo yalitekelezwa, ambapo wamesema kuwa alikatakata  mabaki yake na kupika chakula cha asili cha wali na nyama na kuwapa wafanyakazi ambao ni raia wa Pakistani.

Jaji Mkuu wa Marekani amvaa Rais Trump, adai hakuna jaji wa Obama
Ramaphosa aifagilia Ujerumani

Comments

comments