Binti wa miaka (17), mwanafunzi wa kidato cha pili mkazi wa Kaunti ya Kakamega nchini Kenya, amemuuza mwanaye baada ya kupewa mimba na nduguye wa karibu kisha kufukuzwa kwao.

Taarifa zinasema binti huyo alifukuzwa na baba yake mlezi baada ya kupata ujauzito hivyo mtoto ambaye angezaliwa alionekana kuwa kama ‘laana’ kwa jamii yao na kukiuka tamaduni na desturi zao.

Hata hivyo mama wa binti huyo alilazimika kutafuta mtu wa kumuuzia mtoto, na alilipwa kabla ya binti huyo kujifungua.

Mama wa binti huyo anasema walilazimika kumuuza mtoto kwa kuwa wasingeweza kumlea mtoto huyo na ndiyo sababu wakaamua kumuuza.

Lipuli FC kuanzia Iringa
Kagere awakumbusha Simba SC