Mahakama ya Katiba ya Zimbabwe imetupilia mbali ombi la aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Levi Nyagura akipinga uhalali wa kisheria wa kitengo cha kudhibiti rushwa kusimamia kesi dhidi yake ya kumtunuku shada ya uzamivu Grace Mugabe, Mke wa Rais wa zamani, Robert Mugabe.

Kwa mujibu wa New Zimbabwe, kesi hiyo haikuweza kufanyika Jumatano kama ilivyokuwa imepangwa baada ya Nyagura kuweka pingamizi akidai kuwa kitengo cha rushwa pamoja na mwendesha mashtaka mkuu huteuliwa na Rais, hivyo kuhusishwa kwao hakutamtendea haki.

Aliwataja Tapiwa Godzi na Michale Chakandika kuwa wameingia kwenye kesi hiyo kwa lengo la kumtomtendea haki.

“Mishahara yao inalipwa na Rais; wanasimamiwa na sheria ya siri za maafisa wa serikali,” mwanasheria wa Nyagura, Lewis Uriri anakaririwa na New Zimbabwe.

Hata hivyo, Hakimu Lazini Ncube alikataa maombi ya Nyagura na kueleza kuwa hakukuwa na ushahidi unaoonesha dhahiri ni jinsi gani uhusika wao utaharibu utolewaji wa haki.

Katika kesi ya msingi, inaelezwa kuwa Nyagura hakuwahusisha  wajumbe wa idara ya mambo ya jamii kuhusu maombi ya Grace Mugabe kutaka kuchukua Phd, mwaka 2011.

Pia, Nyagura anadaiwa kuwa alimteua msimamizi wa utafiti kwa ajili ya Grace bila kuijulisha Bodi na kwamba baadaye mwaka 2014, mke huyo wa Rais wa zamani aliiutetea utafiti wake bila kupata idhidi ya kamati ya taaluma.

Mwanakwaya kufia 'gesti' kwazua mengine
JPM atoa siri ya kumtoa bosi Takukuru, Lissu atoboa siri ya dereva wake