Bondia machachari, Terrence Crawford ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya mabondia wawili wenye nafasi ya kupanda ulingoni na bondia bingwa wa dunia na Seneta wa Ufilipino, Manny Pacquiao, amejipa taji la ‘Bondia wa Mwaka 2016’.

Terrence Crawford

Terrence Crawford

Crawford ambaye hajawahi kushindwa pambano, akishinda mapambano yote 30 huku kati ya hayo 20 kwa kumaliza mchezo kabla ya muda (Knock Out), ametumia mtandao wa Twitter kujigamba ikiwa ni siku chache tangu alipompiga kwa knockout John Molina Jr.

Kilichompa kiburi bondia huyo kujitangaza hivyo ni pamoja na namna alivyofungua mwaka kwa kutoa kichapo kizito kwa Henry Lundy kwa knock out katika raundi ya tano mwezi Februari mwaka huu, na mwezi Julai alimshinda kwa alama Viktor Postol ambaye alikuwa akifanya ‘sparing’ na Pacquiao pamoja na kufunzwa na kocha wake, Freddie Roach.

Mbali na Crawford, bondia raia wa Ukrain Vasyl Lomachenko naye anapewa nafasi ya kukutana ulingoni na nguli wa masumbwi, Manny Pacquiao ambaye ametangaza kupanda ulingoni mara mbili katika mwaka 2017.

Video: Yatambue maua yenye sumu msimu huu wa Christmas
Video: Wafanyabiashara masoko ya Dar walia na msimu huu wa Sikukuu