Mbunge, Didmus Wekesa Barasa ambaye ametoroka kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake, ameshinda uchaguzi wa ubunge wa Kilimili kupitia Chama chake cha United Democratic Alliance.

Barasa, anatuhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake Brian Khaemba wa Chama cha DAP-K siki yua Jumanne Agosti 9, 2022 majira ya jioni, alipata kura 26,000 dhidi ya kura 9000 za mpinzani wake Khaemba.

Kiti cha ubunge cha Kimilili pia kilikuwa kikigombaniwa na washindani wengine akiwemo mgombea Peter Makokha wa ODM na Erastus Muchimudi wa Jubilee, ambao hata hivyo hawakujitokeza wakati wa zoezi la ujumlishaji wa matokeo.

Aidha, inadaiwa kuwa kulikuwepo na mchuano mkali katika kituo cha kuhesabia kura za ubunge katika Shule ya Upili ya Wavulana ya St Luke Kimilili siku ya Jumatano Agosti 10, 2022 ambapo Polisi waliimarisha ulinzi.

Trump akataa kujibu maswali kwa kiapo
Kenya: Vigogo waanza 'kunyoosha mikono'