Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimeahirisha mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho uliotarajiwa kujadili hatima ya rais Zuma.

Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho imeeleza kuwa wamekuwa na mazungumzo yenye ufanisi mkubwa na rais Zuma.

Aidha, Rais Zuma yupo katika wakati mgumu kufuatia shinikizo la kumtaka aachie madaraka ambalo linatoka ndani ya chama chake,halikadhalika upinzani.

Taarifa ya Mkutano wa kamati kuu ya chama hicho NEC unatarajiwa kufanyika siku ya februari 17 na 18 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho cha ANC Cyril Ramaphosa.

Hata hivyo, kwa upande wa upinzani wenyewe wameshikilia msimamo wa kumtaka Zuma kupigiwa kura ya kutokuwa na Imani,huku kikao cha kamati kuu kikidaiwa kuwa na nguvu ya kuweza kumuondoa Zuma madarakani hata bila hiari yake.

 

Aliyemuapisha Odinga afukuzwa nchini Kenya
Magazeti ya Tanzania leo Februari 7, 2018