Meneja wa klabu bingwa nchini Ujerumani FC Bayern Munich Carlo Ancelotti ameupa tano uongozi wa mabingwa wa Italia Juventus FC kufuatia usajili waliofanywa kwa mshambuliaji kutoka nchini Argentina Gonzalo Higuain.

Ancelotti aliupa tano uongozi wa kibibi kizee cha Turun, alipokua mgeni maalum katika moja ya vipindi cha TV huko nchini Italia kiitwacho Tiki-Taka, ambapo alisema Juventus wamelamba dume kwa kufanya usajili wa mshambuliaji huyo aliyekua anaitumikia klabu ya SSC Napoli.

Amsema Gonzalo ni mchezaji wa aina tofauti na aliowahi kufanya nao kazi na wakati mwingine hutumia mbinu na maarifa ya ziada kwa lengo la kuisaidia timu yake, hivyo jambo hilo anaamini litaisaidia Juventus katika msimu huu wa ligi.

Meneja huyo kutoka nchini Italia ameongeza kuwa, endapo Juventus wangeshindwa kumsajili Gonzalo angefanya kila njia ya kumpeleka FC Bayern Munich ili akaongeze chachu katika safu yake ya ushambuliaji.

Hata hivyo Anceloti ametoa angalizo kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC kwa kuwaambia wasibweteke na mafanikio waliyoyapata kwa misimu kadhaa iliyopita na badala yake wanapaswa kukaza msuli ili kuendelea kupata mazuri zaidi kwa msimu huu.

Carlo Ancelotti aliwahi kukinoa kikosi cha Juventus kati ya 1999–2001na alifanikiwa kutwaa ubingwa wa UEFA Intertoto Cup mwaka 1999, hivyo amekua mtu wa karibu na klabu hiyo kwa kufuatilia kila hatua wanayoipiga.

PICHA: Serengeti Boys Walivyokamua Jana Tayari Kuwavaa Congo
Arsene Wenger Apambanishwa Na Eddie Howe