Aliyekua meneja wa klabu za AC Milan, PSG, Juventus pamoja na Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa tayari kuirithi nafasi ya Jose Mourinho huko Stamford Bridge.

Ancelotti ameweka wazi utayari wa kurejea jijini London, alipohojiwa na gazeti la Daily Mail usiku wa kuamkia hii leo ambapo amesema hana shaka na suala hilo kutokana na kuamini anaweza kuirejesha katika hali ya ushindani klabu ya Chelsea.

Meneja huyo kutoka nchini Italia, amesema pamoja na kuwa na hali hiyo ya utayari bado maamuzi ya kurejea Chelsea yatatokana na hatua ya kuondoka kwa Jose Mourinho na kisha uongozi kuona kama atakua na umuhimu wa kuirithi nafasi yake.

Ancelotti aliwahi kupita kwenye klabu ya Chelsea kati ya  mwaka 2009–2011, na alifanikiwa kutwaa ubingwa wa nchini England pamoja na kombe la FA, hivyo anaamini kigezo hicho kinatosha kuwashawishi viongozi wa The Blues kwa kuona anafaa kuwa sehemu ya wanaofikiriwa kurithi mikoba ya Mourinho.

Hata hivyo amedai kwamba, hana tofauti zozote za klabu ya Chelsea, licha ya kufukuzwa kwake kazi mwaka 2011, kwa kusema kilichotokea wakati huo ni jambo la kawaida katika ajira ya mtu yoyote.

Ancelotti ndiye meneja aliyerithi mikoba ya Jose Mourinho katika klabu ya Real Madrid mwaka 2013 akitokea PSG, na kama itatokea anachukua ajira huko Stamford Bridge ataweka historia ya kumbadili mreno huyo kwenye klabu mbili tofauti.

Jose Mourinho amekua katika wakati mgumu wa kufikiriwa kama ataendelea kubaki Chelsea kwa msimu huu, kutokana na mwenendo wa kikosi chake kuendelea kuwa mbaya, japo mpaka sasa hakuna taarifa zozote zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo dhidi ya mtu huyo mwenye tabia ya kuzungumza maneno ya kejeli mbele ya vyombo vya habari.

Matunda ya Ziara za Kushtukiza za Rais Magufuli Haya Hapa
Blatter Yu Hoi Hispitalini