Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Paul Ince ameeleza kuwa wachezaji wa kati ya klabu hiyo, Ander Herrera na Marouane Fellaini lazima waondoka Old Trafford.

Akiongea na mtandao wa 888poker, Ince amesema kuwa uongozi wa sasa wa Man United unawapotezea muda na kipaji wachezaji hao na kwamba wanafaa zaidi kucheza soka ya Uhispania.

Paul Ince

Paul Ince

“Sidhani kama Herrera anafaa kuwa kwenye mfumo wa Van Gaal na ingawa ni ni mchezaji mzuri anafaa zaidi kuwa Uhispania. Nilimuona anacheza Uhispania na anatosha kwenye ligi hiyo lakini sidhani kama anatosha kuwa Manchester United. “

Inaelezwa kuwa mfumo anaoutumia Van Gaal unawabana wachezaji hao kuonesha makeke na kipaji chao na kusababisha ndoto za kupata magoli mengi kufifia.

Wakazi Atajwa Kuwania Tuzo Za KORA 2016
ISIS Watoa Vitisho Vipya Kwa Urusi Na Marekani, Watuma Video Wakimchinja Mpelelezi Wa Urusi