Klabu ya Fulham imemsajili kiungo kutoka nchini Ujerumani Andre Schuerrle kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili, akitokea Borussia Dortmund inayoshiriki ligi kuu ya Bundesliga.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, anarejea jijini London, baada ya miaka mitatu, ambapo kwa mara ya mwisho alikua na klabu ya Chelsea aliyoitumikia kuanzia mwaka 2013-15.

Chelsea walimrejesha Schuerrle nchini kwao Ujerumani baada ya kufanya biashara na klabu ya VfL Wolfsburg mwaka 2015, na mwaka mmoja baadae alijiunga na Borussia Dortmund.

“Klabu ya Fulham imekua ya kwanza kuonyesha nia ya kunisajili katika kipindi hiki, niliona kuna umuhimu wa kurejea jijini hapa kutokana na kuyapenda mazingira yake, nina uhakika nitafanya vizuri nikiwa na klabu hii,” Amesema Schuerrle alipohojiwa na mwandishi habari wa tovuti ya klabu ya Fulham.

“Ninapenda kucheza soka la pasi wakati wote, Fulham ni moja ya klabu zinazocheza soka la namna hiyo, hivyo sina budi kujiwekea malengo ili kufanikisha mipango inayokusudiwa klabuni hapa kwa msimu mpya.”

Schuerrle alikua sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2014, lakini hakufanikiwa kuitwa kikosini kwa ajili ya fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Urusi mwaka huu.

Pompeo amkingia kifua Rais Trump
Alphonso Davies aweka rekodi MLS