Mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund Andre Schurrle, atakosa michezo ya awali ya msimu wa Bundesliga, utakaoanza rasmi mwishoni mwa juma hili kufuatia majeraha misuli ya paja.

Mshambuliaji huyo ambaye alikua sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichotwaa ubingwa wa kombe la dunia mwaka 2014, alikua amerejea uwanjani mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa German Cup dhidi ya Rielasingen-Arlen, baada ya kuwa majeruhi kwa majuma kadhaa, na sasa hana budi kujiuguza kwa mara nyingine tena.

“Atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua majuma manne,” Imeeleza taarifa ya klabu.

Hata hivyo kuna wasiwasi kwa Schurrle akaachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kitakachocheza michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za 2018 dhidi ya Jamuhuri ya Czech mjini Prague mnamo Septemba mosi, kisha Norway mjini Stuttgart  Septemba nne.

Hii inatokana na matarajio hafifu ya muda wa kuwa na mazoezi ya kutosha atakapokua amerejea kwenye kikosi cha Borussia Dortmund baada ya kupona majeraha ya misuli ya paja.

Dortmund, walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msiammo wa ligi ya Bundesliga msimu uliopita, na kufuzu moja kwa moja kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu. Wataanza kampeni ya kuwania ubingwa wa Bundesliga kwa kucheza dhidi ya VfL Wolfsburg siku yajumamosi.

Video: Makonda jino kwa jino na makandarasi Dar, asema kiama chao kimefika
Odinga kutinga mahakamani kupinga matokeo