Mchezaji mkongwe wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Andrea Barzagli amewatoa hofu mshabiki wa klabu hiyo, ambao wanahofia huenda pengo la Leonardo Bonucci likashindwa kuzibika.

Leonardo Bonucci aliondoka Juventus Stadium mwezi Juni mwaka huu, na kutimkia mjini Milan baada ya kusajiliwa na AC Milan kwa Euro milioni 42.

Barzagli amesema ni jambo la kushtusha kuona mchezaji kama Bonucci aliyedumu klabuni hapo kwa miaka saba anaondoka katika kipindi hiki muhimu cha kutetea taji lao, lakini akasisitiza bado wana nguvu ya kuwa na safu imara ya ulinzi.

“Ni kawaida kwa mashabiki kupata mshutuko, lakini ni jambo la kawaida ninawasihi wawe watulivu, maana kuondoka kwa Leonardo Bonucci meneja anafahamu nini atakachokifanya ili kuziba nafasi yake.” Barzagli aliliambia jarida la michezo ya Premium Sport.

Hata hivyo Bonucci akagusia suala la kuondoka kwa beki wa pambani kutoka nchini Brazil Dani Alves kwa kurejea wosia kwa mashabiki wa Juventus kuwa watulivu.

“Dani Alves alikua na umuhimu mkubwa kikosini, tangu alipojiunga nasi alionyesha uwezo mkubwa na amesaidia kwa kiasi kikubwa hadi tumefikia hapa tulipo, lakini bado ninawasisitiza mashabiki kuwa na utulivu.

“Kikosi kina wachezaji 23, wanaocheza uwanjani ni 11, hivyo wanaobaki nje wanakua na uwezo mkubwa pia wa kuongezea nguvu, ninawataka mashabiki waamini kama ninavyoamini mimi, tutakua vizuri na tutaweza kutetea taji letu kwa mara nyingine tena.

Dani Alves aliihama Juventus mwezi July baada ya kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliokua umesajilia klabuni hapo, na kujiunga na matajiri wa jijini Paris nchini Ufaransa PSG.

Buhari kurejea nyumbani baada ya matibabu
Valencia CF Yaendelea Kuimarisha Safu Ya Ulinzi