Kiungo na nahodha mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Andres Iniesta, huenda akarejea kikosini mwishoni mwa juma hili kuwakabili Real Madrid katika mchezo wa El Clasico, ambao utachezwa siku ya jumamosi.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, alishindwa kujumuika na wachezaji wenzake tangu Oktoba 22 katika mchezo dhidi ya Valencia, baada ya kuumia goti.

Matarajio ya kurejea kwa kiungo huyo ambaye alikua sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania waliotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2010, yatakua faraja kwa meneja wa Barca Luis Enrique.

Iniesta ameshacheza michezo ya 33 ya El Clasico, na kama atafanikiwa kucheza mwishoni mwa juma hili ataendelea kuwa mchezaji atakeweka historia ya kipekee sambamba na Lionel Messi na Sergio Ramos ambao wameshacheza michezo hiyo mara 32 kwa kila mmoja.

FC Barcelona wapo nyuma kwa point sita dhidi ya vinara wa La Liga Real Madrid, hivyo watahitaji kushinda ili kupunguza pengo la point tatu, ili hali kwa wapinzani wao watakua na kila sababu ya kuendeleza wimbi la ushindi.

Mpaka sasa Real Madrid imeshacheza michezo 31 bila kufungwa.

Casimiro Kuanza Kuivutia Kasi El Clasico
Rais Magufuli: Sitaki Majeshi yaingie ubia na watu binafsi