Kiungo Andrés Iniesta Luján, huenda akatangaza kustaafu soka la kimataifa, baada ya timu yake ya taifa ya Hispania kuondolewa kwenye fainali za Euro 2016, kwa kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Italia.

Iniesta, alisisitiza kuwa katika mustakabali wa kufanya hivyo dakika chache baada ya mtanange wa jana, ambao ulishuhudia wakikubali kuutema ubingwa wa Ulaya ambao waliutwaa mara mbili mfululizo, mwaka 2008 na 2012.

Endapo Iniesta mwenye umri wa miaka 34 atafanya maamuzi ya kuachana na timu ya taifa, atakua akiendeleza kasumba iliyoanzishwa na Lionel Messi  jana alfajiri baada ya kikosi cha Argentina kushindwa katika mchezo wa hatua ya fainali dhidi ya Chile.

Iniesta ni rafiki wa karibu wa Lionel Messi ambaye wanacheza pamoja FC Barcelona.

Hatua ya kusisitiza mustakabali wa kutangaza kustaafu soka la kimataifa, huenda ikawa inampa nafasi Iniesta kutaka ushauri kwa watu wake wa karibu, na pengine rafiki yake Messi huenda akahusishwa katika jambo hilo.

Iniesta, alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa ubingwa wa Euro 2008 na 2012 na pia alitoa mchango mkubwa katika mafanikiwa ya kuibuka vinara wa dunia mwaka 2010 katika fainali zilizofanyika nchini Afrika kusini.

Alianza kuitumikia timu ya taifa ya Hispania mwaka 2006 wakati wa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Ujerumani, na mpaka sasa ameshacheza michezo 113 na kufunga mabao 13.

Picha: Mashabiki Waamkia Uwanja Wa Taifa
Mahakama ya Afrika Kusini Yamkalia Kooni Rais Zuma