Kiungo wa FC Barcelona Andres Iniesta hatokua sehemu ya kikosi kitakachopambana usiku wa leo dhidi ya Real Madrid kwenye uwanja wa Estadio Santiago Bernabeu mjini Madrid.

Iniesta ataukosa mchezo huo wa mkondo wa pili wa kuwania Spanish Super Cup, kufuatia majeraha ya paja aliyoyapata akiwa katika mazoezi ya kujiandaa na mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani.

Iniesta jana alishindwa kufanya mazoezi ya mwisho na wachezajai wenzake, hali ambayo ilidhihirisha hatoweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachokua kwenye harakati za kupindua matokeo ya kufungwa mabao matatu kwa moja ili kufikia lengo ya kutwaa ubingwa wa Spanish Super Cup mwaka huu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33, amekua katika msukosuko wa kupata majeraha ya mara kwa mara tangu msimu uliopita, na kuumia kwake katika kipindi hiki kunamfanya ajiunga na wachezjai wengine walio majeruhi kama Rafinha Alcantara na Thomas Vermaelen.

Pia kuna wasiwasi kwa Iniesta akaukosa mchezo wa kwanza wa ligi msimu huu utakaochezwa mwishoni mwa jua hili, ambapo FC Barcelona watawakaribisha  Real Betis huko Camp Nou.

 

Kamishna wa tume ya uchaguzi Kenya azuiliwa Uwanja wa Ndege
Alexis Sanchez Kuondoka Emirates Stadium 2018