Nahodha na kiungo wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Andres Iniesta, amefichua siri iliyokua ikiendelea kati yake na meneja wa sasa wa Man City Pep Guardiola wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Iniesta amesema Guardiola alionyesha nia ya kutaka kumsajili na kumpeleka Etihad Stadium, lakini alikataa wito huo kwa kuamini England hapakua mahala sahihi kwa soka lake.

Iniesta ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha CF Barcelona wakati Guardiola akiliongoza benchi la ufundi la klabu hiyo kati ya mwaka 2008–2012, amesema lengo lake kubwa kwa sasa ni kutaka kumalizia soka lake akiwa Camp nou.

Hata hivyo amedai kuwa anamuheshimu sana Guardiola na bado ataendelea kuwa mtu wake wa karibu, hivyo amevitahadharisha vyombo vya habari kutolichukua suala la kukataa kwake kwenda Man city kama kuna ugomvi baina yao.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, kwa sasa ni mchezaji mkongwe katika kikosi cha FC Barcelona baada ya kuondoka Carlos Puyol pamoja na Xavi Hernández ambao kwa pamoja walicheza michezo  505 wakiwa Camp Nou.

Iniesta ameshacheza michezo 392 akiwa na FC Barcelona na amebahatika kufunga mabao 34 tangu mwaka 2002 alipopandishwa kutoka kikosi pili hadi kikosi cha kwanza.

Video: Aliyegundua muonekano mpya wa Bodaboda aipongeza Serikali
Polisi Tabora, Geita Gold Zajiongezea Majanga