Kiungo na nahodha wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Andres Iniesta, amekanusha taarifa za kuwa na mpango wa kuihama klabu hiyo ya Camp Nou mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, alidaiwa kuwa katika hatua za mwisho za kuitumikia FC Barcelona, na huenda mwishoni mwa msimu huu akatimkia nchini Marekani ama China kwa ajili ya kwenda kumalizia soka lake.

Iniesta amekanusha taarifa za kuwa mbioni kuihama FC Barcelona, alipohojiwa na kituo cha televisheni cha BeIN Sports, ambapo amesema alishangazwa kuona taarifa hizo katika baadhi ya vyombo vya habari tangu mwishoni mwa juma lililopita.

“Ni vigumu kuondoka hapa, dhamira yangu ni kutaka kuitumikia Barca hadi nitakapostaafu, hizi taarifa za kuwa mbioni kutimkia Marekani ama China zimenishangaza sana,” Alisema Iniesta.

“Baba yangu alinijenga katika misingi ya kuamini ninaweza kupambana, hivyo nitaendelea kupambana hapa ili niendelee kucheza katika kikosi cha kwanza cha Barca. Ninatambua nimesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja na nusu, lakini kuna uwezekano wa kukaa chini na viongozi wangu na nikasaini mkataba mpya.

Klabu ya New York City FC ilitajwa kuwa katika mpango wa kutuma ofa ya usajili wa Iniesta mwanzoni mwa juma hili, kwa kutumia kigezo cha mchezaji huyo kuwa na urafiki na David Villa ili kumshaiwshi ajiunge nae huko Marekani.

Petr Cech Kukaa Nje Mwezi Mmoja
Tanzania na China zasaini mkataba wa utamaduni