Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Andy Cole, ameitabiria mabaya klabu hiyo kwa kusema haitatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England hata kama itawasajili Harry Kane na Declan Rice.

Man United inatajwa kuwa na mpango wa kusajili mkubwa baada ya kufungwa kwenye fainali ya Kombe la FA na Man City, wakati nyota wa Spurs, Kane na kiungo wa West Ham, Rice wakitajwa.

Mail Sport liliandika kuwa Kane anaongoza katika orodha ya wanaotakiwa na Man United, wakati kocha Erik ten Hag akitaka mshambuliaji mpya.

Lakini Cole, mwenye mataji matano ya Ligi Kuu na mshindi wa mataji matatu ya msimu mmoja akiwa na miamba ya Old Trafford, akiltumikia kuanzia 1995 hadi 2001, alisema Man United inahitaji zaidi ya nyota hao wawili ili kuwa bora zaidi,

“Kama Harry Kane anataka kuondoka Tottenham na Man United inataka kutumia zaidi ya Pauni 80 milioni kwa mchezaji mwenye miaka 29, shauri yao,” Cole alllambla BoyleSports.

Filamu: Wadau hawafuati taratibu - Dkt. Chana
Pombe: Wanane wauawa kwa risasi, wawili wajeruhiwa