Bingwa wa Dunia wa uzito wa juu, Andy Ruiz Jr, amemtambia Anthony Joshua kwa kusema kuwa sio bondia mzuri akiwa ulingoni na hata wakirudia mechi atamchapa tena.

Kibonge mwepesi huyo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kuwa na tetesi kuwa wawili hao wanataka kuzichapa kwa mara nyingine.

“Nishajua makosa yake, naweza kufanya kitu bora zaidi, kitu pekee anachoweza yeye ni kukimbiakimbia uwanjani, sio mzuri akiwa ulingoni tukirudia itakuwa vilevile,”amesema Ruiz

Aidha, Andy Ruiz Jr, amepata umaarufu mkubwa sana baada ya kumchapa bondia, Anthony Joshua katika raundi ya saba katika mchezo uliopigwa Juni 1.

Hata hivyo promota wa bondia Anthony Joshua, amesema kuwa wawili hao wanaweza kuzichapa tena Novemba 16 au Decemba 14 mwaka huu.

 

Kibiti yahusishwa mauaji ya Watanzania 9 Msumbiji, Sirro atuma salamu kwa Wauaji
Waziri Kairuki ahimiza ushirikiano kati ya kiwanda na wananchi