1. Joe Louis
Ni raia wa Marekani. Alishinda mapambano 66 ambapo kati ya hayo 52 yalikuwa kwa KO.. Katika historia yake alipoteza mapambano matatu tu. Wamarekani wanamkumbuka kwa namna mapambano yake yalivyosaidia kuleta utulivu wakati wa vita vya pili vya dunia.

2. Muhammad Ali
Alipigana kati ya mwaka 1960 hadi 1981 akishinda mapambano 56 ambapo kati ya hayo 37 yalikuwa kwa KO. Alipoteza mapambano matano pekee. Wamarekani wanamkumbuka kwa ngumi zake zilizotaliwa na burudani.

3. Sugar Ray Leonard
Alipigana kati ya mwaka 1940 na 1965 na kushinda mapambano 173 ambapo kati ya hayo 109 yalikuwa kwa KO.

4. Jack Johnson
Huyu jamaa alikuwa katili usiambiwe na mtu. Mara nyingi alipenda wapinzani wake waendelee kuwa ulingoni ili awapige. Hakutaka kabisa wapige chini kama ishara ya kushindwa. Alishinda mapambano 73 kati ya 1897 na 1945 ambapo 40 yalikuwa kwa KO.

5. Jack Dempsey
Alishinda mapambano 66 ambapo kati ya hayo 51 yalikuwa kwa KO. Mmarekani huyo alipoteza mapambano sita tu.

6. Mike Tyson
Alipigana kati ya 1985 na 2005. Kuna nyakati alipigana kwa miaka 10 bila kupoteza pambano. Alishinda mapambano 50 ambapo 44 yalikuwa mwa KO. Alipoteza mapambano sita pekee.

7. Julio Cesar Chavez Jr
Alipigana kati ya 1980 hadi 2005 akishinda mapambano 107 ambapo kati ya hayo 80 yalikuwa kwa KO. Raia huyo wa Mexico mbali na ushindi alisifika pia kwa ngumi zilizoambatana na burudani.

8. Rocky Marciano
Alipigana kati ya 1948 na 1955 akishinda mapambano 49 ambapo kati ya hayo 43 yalikuwa ya KO. Hakuwahi kupoteza pambano hata moja. Lakini nyakati zake hazikuwa na ushindani mkubwa.

9. Henry Armstrong
Alipigana kati ya 1931 na 1945 akishinda mapambano 150 ambapo 100 alishinda mwa KO. Alipoteza mapambano 21.Aliwahi kushinda mapambano 27 mfululizo.

10. Willie Pep  

Alipigana kati ya 1940 hadi 1966 akishinda mapambano 229 ambapo 65 ni kwa KO. Alipoteza mapambano 11.

Simba Kukwea Kileleni Baada Ya Miaka 3
Ommy Dimpoz amvaa Nay Wa Mitego, Ni baada ya kudai 'Jogoo hawiki'