Mtandao wa Sokkaa.com, umefanya uchunguzi wa kina na kubaini wachezaji watano waliowahi kuwika dunia wakiwa na timu zao za taifa pamoja na klabu, lakini waliathiriwa kwa kiasi kikubwa na ulevi.

Mtandao wa Sokkaa.com umekua ukifanya uchunguzi na kuibua mambo ya kustaajabisha na kufurahisha yanayowahusu wanasoka duniani.

Katika orodha hiyo Sokkaa.com wametoa majina ya wachezaji watano ambao wameonekana wanatosha kuingia katika rekodi ya kutumia vilevi, na wakati mwingine kuwaathiri hadi kupoteza muelekeo wa kimaisha ama kupoteza maisha kabisa.

5: George Best

Huyu alikua mshambuliaji hatari wa timu ya taifa ya Ireland ya kaskazini na klabu ya Manchester.

Alifanikiwa kutamba kwa kupachika mabao muhimu na maridadi akiwa na timu yake ya taifa na klabu ambayo ilimkuza na kumpandisha chati duniani, Man Utd.

Alitamba kati ya mwaka 1963-1984, akiwa na klabu mbali mbali lakini pamoja na kuwa lulu uwanjani, aliathiriwa sana na ulevi wa kupindukia.

Best, alipata athari kimwili kutokana na ulevi wa pombe na ilipofika mwaka 2002 alibainika kuwa na matatizo ya ini ambayo yalisababishwa na pombe kali alizokua akinywa.

Mwaka 2005, Best alifariki dunia kutokana na matatizo ya kiafya yaliyotokana na ini lake kushindwa kufanya kazi kabisa.

Akiwa na klabu ya Man Utd, Best alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini England mara mbili, ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mara moja, huku akicheza michezo 474 na kufunga mabao 181.

 

  1. Paul Gascoigne

Huyu alijulikana kwa jina la utani la Gazza, alitamba katika medani ya soka katika miaka ya 80 na 90 akiwa na timu ya taifa ya England.

Yupo hai mpaka sasa, lakini alijiingiza katika masuala ya matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ulevi wa kipundukia, hali ambayo ilimfanya atengwe na watu wake wa karibu.

Wakati mwingine Gazza alifikia hatua ya kupoteza fahamu na kupelekwa katika vituo maalum vya afya huko nchini England, kutokana na ulevi wa kupindukia.

Aliwahi kucheza katika baadhi ya klabu za soka kama Newcastle United, Tottenham Hotspur, Lazio, Rangers, Middlesbrough, Everton, Burnley, Gansu Tianma pamoja na Boston United na kwa upande wa timu ya taifa alicheza kuanzia mwaka 1988–1998.

Kwa upande wa klabu alizozitumikia Gazza alifanikiwa kufunga mabao 110 katika michezo 468 aliyocheza.

 

  1. Tony Adams

Huyo alikua nahodha na beki mashuhuri wa klabu ya Arsenal na mpaka sasa anaendelea kusheshimika kwenye klabu hiyo kutokanana mazuri na makubwa aliyoyafanya.

Amekua muathirika wa ulevi wa pombe, japo jamii ya watu wanaomzunguuka kuendelea kumuheshimu kutokana na muonekano alionao kwenye jamii.

Hata hivyo aliwahi kuonyesha vituko vya kunywa katika sehemu za starehe mpaka akaanguka, na kuukotwa na watu wake wa karibu na kumpeleka nyumbani

Aliwahi kutamba akiwa na timu ya taifa ya England, na alianza ulevi tangu mwishoni mwa miaka ya 80.

Akiwa na klabu ya Arsenal alicheza michezo 504 na alifunga mabao 32.

 

  1. Adriano Leite Ribeiro

Sote tunamkumbuka, mtu huyu kutoka nchini Brazil. Lakini sababu kubwa iliyomuondoa katika medani ya soka ni ulevi wa kupindukia pamoja na kupenda sana wanawake.

Akiwa katika utendaji wake uwanjani, alikua mtu mwenye kujituma wakati wote na alionyesha dhamira ya kutaka kufika mbali, lakini ilishindikana kutokana na udhaifu wa ulevi.

Tangu alipoanza kucheza soka na kupita katika klabu za Flamengo, Internazionale, Fiorentina, Parma, São Paulo, Flamengo, Roma,Corinthians pamoja na Atlético Paranaense alifanikiwa kufunga mabao 176 katika michezo 394.

Kwa upande wa timu ya taifa alicheza michezo 48 na kufunga mabao 27.

  1. Diego Maradona

Hakuna asiyemfahamu Diego Maradona, kutokana na historia kubwa aliyojiwekea katika medani ya soka ulimwenguni kote, hususana katika fainali za kombe la dunia za mwaka 1986 pamoja na 1990.

Kila mmoja wetu alimpenda kufuatia mambo mazuri aliyokua akiyaonyesha uwanjani, lakini wakati fulani baadhi yetu tulipunguza mapenzi dhidi yake kutokana na kujiingiza katika ulevi wa kutumia dawa za kulevya na pombe kali.

Alifikia hatua hadi ya kutimuliwa na FIFA, wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 1994, baada ya kubainika alitumia dawa za kusisimua misuli.

Katika historia yake inaonyesha waliwahi kuzichezea klabu ya Argentinos Juniors, Boca Juniors, FC Barcelona, SSC Napoli, Sevilla pamoja na Newell’s Old Boys.

Alifanikiwa kufunga mabao 259 katika michezo 491 aliyocheza upande wa klabu hizo, lakini kwa upande wa timu yake ya taifa alicheza michezo 115 na kufunga mabao 47.

Fainali BSS 2015: Kayumba Ashinda Shilingi Milioni 50
UEFA Wabariki Adhabu Ya Bosi Wao