Wenyeji wa fainali za mataifa bingwa barani Afrika (CHAN 2020) Cameroon, wataanza mchakato wa kusaka ubingwa wa fainali hizo kwa kupapatuana na Zimbabwe Aprili 04.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na shirikisho la soka barani Afrika CAF, mchezo huo wa ufunguzi umepangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Ahmadou Ahidjo ambao pia utatumika kwa ajili ya mchezo wa mwisho (Fainali) Aprili 25.

Kwa upande wa mabingwa watetezi wa fainali za CHAN Morocco, wataanza harakati za kutetea ubingwa wao dhidi ya Togo Aprili 06, kabla ya kuzikabili Rwanda na Uganda katika michezo ya kundi C.

Ratiba kamili ya michuano ya CHAN 2020.

Image result for chan 2020 fixture

 

Serikali yashusha rungu kwa madalali, usajili
Jorginho ahimiza mapambano dhidi ya Bayern Munich

Comments

comments