Meneja mpya wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou ametamba kwamba anataka kurudisha soka tamu na la kushambulia kwenye klabu hiyo yenye maskani yake London.

Ange ametua Spurs kuchukua mikoba ya Antonio Conte na amesainishwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi, lakini saini yake ikinaswa kwa Celtic kulipwa fidia ya Pauni 5 milioni.

Kibarua chake cha kwanza huko Spurs kitakuwa ni kumshawishi kinara wa mabao wa timu hiyo, Mshambuliaji Harry Kane asiondoke, wakati huu akiwindwa na klabu za Real Madrid na Manchester United.

Spurs imekuwa na historia ya kuwa na washambuliaji matata sana kama Cliff Jones, Ossie Ardiles, Glenn Hoddle, Paul Gas- coigne na Gareth Bale na sasa Ange anataka kurudisha makali ya timu hiyo kwenye ishu ya ushambuliaji.

Spurs wamemnasa Postecoglou baada ya kuvutiwa na huduma yake kwa kile alichokuwa akifanya Celtic akibeba mataji ya kutosha huko Scotland.

Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy baada ya kujaribu kuwanasa Arne Slot, Julian Nagelsmann na Vincent Kompany na kuwakosa huku Mauricio 57, atakuwa mtu sahihi kuja kufanya kazi kwenye klabu yake.

ambayo ilishuhudiwa makocha wengi mahiri kama Jose Mourinho na Nuno Espirito Santo wakishindwa kuipa mafanikio timu hiyo ambayo haijatwaa taji lolote tangu 2008.

Wizara ya Fedha yaomba Bunge kuidhinisha Trilioni 15
Otile Brown, Meneja Noriega 'wamwagana' rasmi