Mfungaji wa bao la ushindi katika mchezo wa Fainali kati ya Argentina dhidi ya Brazil Angel Di Maria, ameweka wazi alichozungumza na Lionel Messi baada ya mchezo huo.

Argentina iliibuka Mabingwa wa Michuano hiyo mwaka 2021, leo alfajiri kwa kuwafunga wenyeji Brazil bao 1-0, Uwanja wa Maracana mjini Rio de Janairo.

Di Maria ambaye ni Mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa amesema, baada ya dakika 90 za mchezo huo, Messi alimfuata na kumshukuru kwa kufanikisha ushindi kwa taifa lao.

Amesema Nahodha na Mshambuliaji huyo wa FC Barcelona, pia alimshukuru kwa kumuwezesha yeye binafsi na wachezaji wengine kufikia ndoto za kuwa mabingwa baada ya miaka mingi kupita.

“Haiwezi kusahaulika, Messi amenishukuru na amenieleza kwamba ilikuwa fainali yangu, sidhani kama inaweza kujirudia, ilikuwa ni leo na mambo ndio kama yalivyokuwa.”

“Ninafurahi kwa binti zangu, mke wangu, wazazi wangu na watu wote waliotuunga mkono kwa kutusapoti.”

“Kombe la Dunia linakuja hivi karibuni, tunapaswa kufunga kamba za viatu vyetu kwa ajili ya mapambano mengine mbele yetu.” amesema Angel Di Maria.

Mchezo wa jana ulikua Fainali ya tano kwa Argentina, na mara nne zilizopita waliishia kumwaga machozi kwa kukosa ubingwa.

Mara tatu kati ya hizo Argentina ilikosa ubingwa wa Copa America mara tatu na mara moja ilikua ubingwa wa Kombe la Dunia.

Rais Samia atuma salamu za pole na kutoa agizo kwa vyombo vya usalama
Sarpong arejeshwa kundini