Muigizaji wa kike, Angelina Jolie amezungumzia kuhusu mpango wa kuingia kwenye siasa katika siku za usoni, akieleza kuwa alikuwa na mpango tofauti miaka 20 iliyopita.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na kipindi cha BBC Today, muigizaji huyo wa Mr. &Mrs Smith, alisema kuwa miaka 20 iliyopita angeulizwa kuhusu mpango wa kuingia kwenye siasa angebaki anacheka tu na angedhani labda swali hilo lilikuwa utani, lakini hivi sasa ni tofauti.

“Kama ungeniuliza swali hili miaka 20 iliyopita, ningeishia kucheka tu…. Siku zote nimekuwa nafahamu ninapotaka kwenda, na sikujua kama ninatosha kwenye siasa… lakini kwa wakati huo nilikuwa nikitania kuwa sijui kama nina mifupa iliyobaki,” alisema Jolie.

“Nina uwezo wa kufanya kazi na Serikali lakini pia nina uwezo wa kufanya kazi na jeshi, na ninakaa kwenye maeneo mengi ambayo yananiwezesha kukamilisha kazi husika,” aliongeza.

Alipoulizwa kama atakuwa mmoja kati ya watu watakaoshiriki kinyang’anyiro cha chama cha Republican kuwania kupewa nafasi ya kugombea urais wa Marekani, hakujibu na badala yake alishukuru kwa kufikiriwa kuwa katika nafasi hiyo. “Asante,” alisema.

Jolie ambaye amekuwa mjumbe wa Wakala wa Umoja wa Mataifa wa Kushughulikia Wakimbizi, amefanya kazi pia katika kampeni za kupinga unyanyasaji wa kingono pamoja na matatizo yanayowakabili wakimbizi.

Pia, ameshiriki katika kusaidia wasichana wanaoishi katika mazingira magumu hususan kwenye nchi ambazo zilikumbwa na vita, ili wapate elimu bora na bure.

Hivi sasa amepata nafasi ya kufanya kazi kwenye kituo cha BBC ambapo atakuwa mmoja wa watayarishaji wa kipindi cha watoto ambacho kitaanza kuoneshwa Januari mwakani.

Serikali ya DRC yamtimua balozi wa Umoja wa Ulaya
Masha ajibu mapigo kuhusu Fastjet, 'kwasasa nipo tayari'