Badala ya kuinua vidole vya kebehi kwa kile ambacho Young Africans wanapitia, ni wakati mzuri wa kujifunza kupitia wao ili makosa kama haya yasirudie tena ndani ya nchi hii.

1. Nchi inahitaji mfumo bora wa soka la kisasa kuanzia ngazi ya taifa mpaka chini.

2. Nchi inahitaji viongozi sahihi wenye uelewa mpana wa soka katika usimamizi na uendeshaji wake.

3. Nchi inahitaji kuutambua mchezo huu kama chanzo sahihi cha ajira , kodi kwa serikali na muktadha sahihi wa idara nyingine nje ya soka kuwekeza.

4. Nchi inahitaji kuweka sera ya kitaifa kuhusu maendeleo ya mchezo huu katika awamu mbalimbali.

5. Kama taifa linahitajika kuutazama mchezo huu kama sehemu ya fahari ya nchi hii itaruhusu pia vyombo vyake vya dola kusimamia uongozi bora kwa maana ya kukataa rushwa na hongo. Rushwa , hongo na utakatishaji fedha vinasimama kama miba michungu ya maendeleo ya mpira huu.

Leo wanachama, viongozi, wapenzi na wadau mbalimbali wanaicheka Yanga lakini makosa kama haya haya yatajirudia tena kwa timu nyingine na mwendelezo wa kudorola kwa soka la nchi kuendelea.

Kilichowaponza Young Africans ni kukosa uongozi bora , utegemezi uliopindukia , kushindwa kuwa na utayari wa maandalizi ya kati na mbali , kujitathimini na mengineyo mengi. Hivyo basi wengine na Yanga wenyewe waitumie klabu hii kama reference ili kujipanga vyema kwa mustakabali mzuri mbeleni.

Anguko la jabali lina kishindo kikuu lakini kishindo hicho kiwe ‘ wake up call ‘ kwa kesho yenye neema.

Seleman Nonga, Dadu Fadhil Msemo waondolewa RCL
Hatma mgomo wa wahadhiri kujadiliwa leo