Mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Bi. Anna Mghwira amewataka wananchi kuhakikisha wanafanya mabadiliko ya kweli kupitia vyama vya upinzani na kukikataa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai kuwa kimeoza.

Akihutubia katika mkutano wa Kampeni mjini Masasi, Bi. Mghwira aliwaeleza wananchi kuwa CCM imechoka na inafahamu hilo kwa kuwa hata viongozi wakubwa wa chama hicho wamekuwa wakitamka hadharani hivyo wananchi wasikubali kufuata sanaa za sinema wanazofanyiwa na wagombea wa chama hicho katika kampeni.

“Chama Cha Mapinduzi nafikiri kimedumu kwa muda wa kutosha, hata kama wana chama cha mapinduzi na wao wako hapa na wao wanelewa jinsi ambavyo ndani kulivyo kubaya. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kila siku anatutangazia jinsi ambavyo chama chake kimeoza kwa rushwa,” alisema.

“Watu wanakuja kutuchezea sinema hapa tunawaangalia tunawapa ridhaa wanaendelea kutuchezea tena miaka nenda miaka rudi, huu ni wakati wa kubadilika,” aliongeza.

Bi. Mgwira aliwataka wananchi wa Masasi kumchagua kuwa rais wa Tanzania kwa kuwa ataweka sera nzuri zitakazowasaidia kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo cha Korosho.

Picha: Lowassa Ateka Ngome Nyingine Ya CCM
Mahakama Kuu Yatengua Hukumu Dhidi Ya Mbowe