Mgombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Bi. Anna Mghwira amevitaka vyama vya upinzani kuwa kitu kimoja na kuacha kushambuliana kwa kuwa wote wana lengo la kukiondoa madaraki Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mgombea huyo wa urais aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mbulu.

Kadhalika, aliwataka wananchi kutowapigia kura wagombea wa CCM kwa ngazi zote kwa madai kuwa mfumo wa chama hicho umeshindwa kuwaletea wananchi maendeleo.

“Siku ya kura jamani, tukiweke kando hiki chama kwanza [CCM], tukiweke kando pamoja na mgombea wao. Tuviangalie vyama vya upinzani. Na vyama vya upinzani ni kitu kimoja, tusianze kunangana majukwaani. Tukumbuke kwamba sisi sote tumejianzisha baada ya kuona mfumo uliopo hautoshelezi,” alisema.

Katika hatua nyingine, mgombea huyo aliwaahidi wananchi kuwa endapo atachaguliwa kuwa rais atahakikisha kuwa ndani ya siku 100 anarudisha bungeni mchakato wa Katiba Mpya na kwamba atampa Jaji Joseph Warioba nafasi ya kumalizia kazi yake.

Unashindwa Kuweka Akiba Ya Kipato Chako Kidogo? Tumia Njia Hizi
Angalia Video Mpya ya Vanessa Mdee – Never Ever