Bondia Muingereza, Anthony Joshua amefanikiwa kutetea mkanda wake wa ubingwa wa IBF uzito wa juu baada ya jana usiku kumzima katika raundi ya tatu Eric Molina katika pambano lililofanyika jijini Manchester, Uingereza.

Joshua alifanikiwa kumpiga kwa TKO Molina katika raundi ya tatu ya pambano hilo baada ya kuachia sumbwi zito lililomzidi nguvu mpinzani wake, hali iliyopelekea muamuzi kuingilia kati na kumaliza pambano hilo.

joshua-speed

Kutokana na ushindi huo, Joshua mwenye umri wa miaka 27 ambaye hajawahi kushindwa akiwa anashinda kwa TKOs mara 18, amefuzu kupambana na bondia mbabe wa zamani aliyebatizwa jina la ‘Mfalme’, Wladmir Klitschko, pambano litakalofanyika katika uwanja wa Wembley, Aprili 29 mwakani.

Klitschko alikuwa anashuhudia pambano hilo karibu na uringo na alimpongeza bondia hiyo.

joshua-na-klitschko

Wladmir Klitschko na Anthony Joshua

“Huku ndio kupiga hatua ambako watu walikuwa wanataka,” Joshua alisema. “Klitschko anataka kurudisha mkanda wake, na bondia bora zaidi kati yetu atashinda,” aliongeza.

Klitschko mwenye umri wa miaka 41 alipoteza ubingwa wake kwa Tyson Furry ambaye hata hivyo alivuliwa mikanda yote baada ya kukumbwa na kashfa za kutumia dawa za kuongeza nguvu na dawa za kulevya. Furry alitangaza kuachana na masumbwi na kueleza kuwa anajuta kujihusisha na mchezo huo.

Pambano la Joshua na Klitschko ni moja kati ya mapambano yatakayovuta mashabiki wengi na huenda kurejesha kwa kasi ile nguvu ya mvuto wa masumbwi ya uzito wa juu.

 

CUF wamtaka Mwigulu Nchemba na Naibu wake kujiuzulu
Ali Kiba afunika tuzo za EATV, angalia orodha kamili