Uongozi wa klabu ya Manchester United umeanza kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa pembeni kutoka Ufaransa Anthony Martial, ili kukamilisha mipango ya kumsainisha mkataba mpya.

Martial mwenye umri wa miaka 22, amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo, na tayari alikua ameonyesha nia ya kutaka kuondoka katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa majira ya kiangazi.

Wakala wa mshambuliaji huyo, aliwahi kukarriwa na vyombo vya habari akisema kuwa, mchezaji wake anahitaji kucheza mara kwa mara, hivyo ni bora akaondoka Man Utd na kwenda mahala pengine, ambapo ataweza kufikia malengo ya kuwa kwenye kikosi cha kwanza.

Klabu ya Tottenham ilionyesha nia ya kutaka kumsajili, lakini ombi lao liliwekewa pingamizi na meneja Jose Mourinho, ambaye alidai bado anamuhitaji mshambuliaji huyo, katika kikosi chake.

Martial pia aliwahi kutaka kutumiwa kama chambo wa kufanikisha dili la kupatikana kwa wachezaji Willian wa Chelsea na Ivan Perisic Inter Milan, lakini bado mpango huo haukufanikiwa.

Hata hivyo harakati za mazungumzo yaliyoanza baina ya uongozi na mshambuliaji huyo, bado zipo katika maswali yanayokosa majibu, kutokana na hitaji la Martial kuhitaji kucheza katika kikosi cha kwanza.

Endapo jambo hilo litashindikana, huenda mshambuliaji huyo akaondoka mwezi Januari mwaka 2019 wakati wa dirisha dogo la usajili, na kama itashindikana ataondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu wa 2018/19.

Martial alisajiliwa na Man utd kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 36 akitokea AS Monaco ya Ufaransa mwaka 2015, na kwa msimu huu amecheza mchezo moja dhidi ya Brighton, uliomalizika kwa Man Utd kufungwa mabao matatu kwa mawili.

Katika mchezo wa mwanzoni mwa juma hili ulioshuhudia Man Utd wakicharazwa bakora 3-0, mchezaji huyo hakuwa sehemu ya kikosi kilichopata aibu hiyo kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Trafford.

Mwamunyange ateuliwa na Rais wa Zimbabwe
Ratiba ya ziara za Rais Magufuli mwezi Septemba