Mshambuliaji kutoka nchini Ufaransa Anthony Martial, ameonyesha kuwa tayari kurejea kwenye meza ya mazungumzo na uongozi wa klabu ya Man Utd, ili kukamilisha dili la kusaini mkataba mpya.

Martial, ameonyesha utayari huo, kufuatia kuridhishwa na hatua za kutumika kwenye kikosi cha Jose Mourinho, tofauti na ilivyokua msimu uliopita na mwanzoni mwa msimu huu.

Mkataba wa sasa wa mshambuliaji huyo aliyejiunga na Man Utd mwaka 2015 akitokea AS Monaco ya nchini kwao Ufaransa, utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Awali alikua katika mazungumzo na uongozi wa Man Utd, lakini masharti ya kutaka kuingizwa kwenye kikosi cha kwanza, yalikua chagizo la kusitishwa kwa hatua hiyo, kutokana na msimamo wa Mourinho, ambaye aliwahi kusema hatokua tayari kuingiliwa katika mipango yake kwa matakwa ya mchezaji.

Wakala wa Martial amevieleza baadhi ya vyombo vya habari nchini England kuwa, wakati wowote kuanzia sasa watarejea katika meza ya mazungumzo na uongozi wa Man Utd, ili kukamilisha dili la kusianiwa kwa mkataba mpya wa mchezaji wake.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mkataba mpya wa Martial utamuwezewa kulipwa mshahara wa Pauni 200,000 kwa juma, kutoka 150,000 kwa juma anaolipwa sasa.

JPM na JK wafanya mazungumzo Ikulu
Wakulima waitaka serikali kupeleka Wataalam wa Kilimo