Beki kutoka nchini Brazil David Luiz, anatarajiwa kucheza kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi cha Chelsea msimu huu, baada ya kurejea Stamford Bridge mwishoni mwa mwezi uliopita akitokea kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa PSG.

Luiz ataanzishwa katika kikosi cha kwanza cha The Blues, kwa lengo la kuziba nafasi ya beki John Terry ambaye kwa sasa anauguza majeraha ya kifundo cha mguu alioyapata wakati wa mchezo wa ligi ya England dhidi ya Swamsea City mwishoni mwa juma lililopita.

Meneja wa Chelsea Antonio Conte, amethibitisha mpango wa kumtumia beki huyo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Liverpool utakaochezwa jijini London siku ya ijumaa.

“David Luiz atakua sehemu ya wachezaji nikaowaanzisha siku hiyo” alisema Antonio Conte.

“Kama umemsajili mchezaji katika kipindi fulani, itakulazimu umpe muda ili aweze kuzoea mazingira yanayomzunguuka, lakini kwa Luiz naamini atacheza vizuri kwa sababu anapafahamu hapa,

“Alicheza kwa kujituma wakati akiwa na Chelsea kwa miaka mitatu na hata alipokua (PSG) alionyesha uwezo mkubwa, hivyo ninamuamini katika majukumu ambayo ninatarajia kumpa wakati wa mchezo dhidi ya Liverpool.” Aliongeza Conte

Luis mwenye umri wa miaka 29 aliondoka Chelsea miaka miwili iliyopita chini ya utawala wa Jose Mourinho na aliuzwa nchini Ufaransa kwa kiasi cha Pauni milioni 50.

Kwa mara ya kwanza Luiz alijiunga na Chelsea mwaka 2011 kwa ada ya Pauni milioni 21, akitokea nchini Ureno alipokua akiitumikia klabu ya Benfica.

Kwa kipindi cha miaka mitatu aliyokaa Stamford Bridge, alicheza michezo 143 na kufanikiwa kufunga mabao 12.

Roy Keane: Guardiola Anapaswa Kuitwa “The Special One”, Sio Mourinho
Kiev Kuwa Mwenyeji Wa Fainali Ya UEFA 2018