Mwanamke mmoja nchini India amenusurika kifo mara baada ya kupambana na Chui kwa ajili ya kumuokoa mbuzi wake ili asiliwe na Chui.

Rupali Meshram, mwenye umri wa miaka 23, amesema kuwa alipomsikia mbuzi wake akilia ,alikimbilia nje ya nyumba yake iliyopo jimbo la Maharashtra magharibi.

Amesema kuwa baada ya kumuona Chui huyo alichukua fimbo na kuanza kumtandika yule chui, ambaye alimshambulia yeye na Mama yake na kuwajeruhi lakini wote waliweza kujiokoa na mnyama huyo mkali.

Aidha, wawili hao, wote walikutwa na majeraha madogo madogo nawalitibiwa hospitalini na kuruhusiwa lakini mbuzi wao hakunusurika.

Hata hivyo, Kijiji chao huwa kinavamiwa mara kwa mara na wanyama pori kwa sababu kipo jirani na hifadhi ya wanyama pori.

 

 

Magazeti ya Tanzania leo Aprili 5, 2018
Mashabiki, Wanachama Young Africans watakiwa kusahau yaliyopita

Comments

comments