Mtu mmoja aliyepandisha mapepo amewaua waumini wawili wa kanisa la Siloam waliokuwa wakibatizwa katika mto Ungwasi wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Mkuu wa wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea jana majira ya saa sita mchana.

Alisema kuwa wakati waumini hao wakibatizwa kwenye kina kirefu, mtu huyo aliyekuwa miongoni mwao alipandisha mapepo na kumshikilia mmoja akimkandamiza kwenye maji ya mto huo yenye kina kirefu, na kwamba baada ya kuona tukio hilo, muumini mwingine aliamua kumsaidia aliyebanwa na mtu huyo mwenye mapepo lakini aliwashikilia wote wawili ndani ya maji hadi walipopoteza maisha.

Kwa mujibu wa Mwananchi, mkuu huyo wa wilaya alisema kutokana na tukio hilo, jeshi la polisi linawashikilia watu watatu akiwemo mchungaji wa kanisa la Siloam aliyekuwa anafanya ubatizo huo.

50 Cent atamba kumficha Jay Z mwishoni mwa mwaka na albam mpya
Raila afunguka kama atakubali matokeo akitangazwa kushindwa

Comments

comments