Makamu wa rais wa zamani nchini Zimbabwe, Joice Mujuru ameshambuliwa kwa mawe wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa siasa

Chama cha upinzani cha Mama Mujuru cha National People’s Party kimesema Bi Mujuru na wanachama wengine walishambuliwa kwa mawe walipokuwa wakifanya mkutano wa kampeni katika viunga vya mji wa Harare.

Aidha, kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji BBC limesema kuwa msemaji wa chama hicho ameweka wazi kwamba mama Mujuru amejeruhiwa kidogo huku taarifa kutoka ndani ya chama ikisema watu wanane walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Taarifa ya chama hicho imesema shambulio hilo lilikuwa la kisiasa na lilifanywa na wanachama wa chama tawala cha Zanu-PF Party.

Hata hivyo, Rais wa sasa wa nchi hiyo’ Emmerson Mnangagwa ameahidi kufanyika kwa uchaguzi nchini humo ili kuwabaini wahusika.

 

Magazeti ya tanzania leo Februari 3, 2018
Katambi: Ubabaishaji wa Chadema ndio ulinifanya nihame