Kampuni ya Apple sasa inaandaa aina mpya ya iPhone ambayo serikali yoyote duniani haitaweza kuidukua kwa lengo la kupata taarifa za mawasiliano za mteja wa simu hizo.

Taarifa ya maandalizi hayo zimeripotiwa kwa mara ya kwanza na ‘New York Times’ zimeeleza kuwa kampuni hiyo ya Marekani imechukua uamuzi huo baada ya kuwepo mvutano mahakamani kati yake na FBI inayotaka kupata fursa ya kudukua iPhone ya Syed Farook aliyefanya tukio la kigaidi San Bernardino nchini humo.

FBI inataka Mahakama kuwalazimisha Apple kuruhusu FBI kupekuwa simu ya mshambuliaji huyo kwa kutoa ukomo wa namba ya siri ambayo mtu anaweza kuweka kwa lengo la kutaka kuifungua simu hiyo, ili waweze kujaribu hadi kuifungua simu hiyo.

Hata hivyo, Apple wameweka msimamo mkali wakidai wanalinda haki ya ‘faragha’ ya mtu huyo ambaye kwao alikuwa mteja.

Uliwahi kuipenda Hesabu? Leo ni siku ya Pie '22/7' duniani
Picha: Ni Mafuriko Mahakamani, Kesi ya Wenje kupinga ushindi wa Mabula