Wakati michuano ya kombe la dunia ikitarajiwa kupigwa nchini Urusi mwaka 2018 tayari baadhi ya nchi zimekwishaanza kupigana vikumbo kwa ajili ya kuwa wenyeji wa michuano hiyo mwaka 2030.

Marais watatu Horacio Cartes wa Paraguay, Maurcio Macri wa Argentina na rais wa Uruguay Tabare Vazquez waliweka kikao kwa pamoja na kujadili mambo mbali mbali ya mataifa hayo na ndipo wakaja na hoja moja ya kuungana kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa duniani mwaka 2030.

Wakati Argentina, Uruguay na Paraguay wakijipanga kuaandaa mashindano hayo, huko barani Asia nchi ya China nayo imeonesha matamanio ya kuandaa michuano hiyo mikubwa duniani.

Mbali na China shirikisho la soka barani Ulaya UEFA mwezi Julai mwaka huu walisema watawapa ushirikiano mkubwa Uingereza kuandaa michuano hiyo.

Michuano ijayo ya kombe la dunia itapigwa nchini Urusi mwakani huku baada ya hapo taifa la Qatar litaandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 na kisha Mexico – USA na Canada wakijipanga kwa 2026 ambapo Morocco nao wanataka kuandaa michuano hiyo.

 

RC Rukwa atoa onyo kali kwa madereva
DC Hapi atishia kufuta leseni za wamiliki wa hoteli