Mabingwa wa kihistoria duniani timu ya taifa ya Brazil, wameendelea kutesa katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, baada ya kuibanjua timu ya taifa ya Argentina mabao matatu kwa sifuri.

Mchezo wa miamba hiyo ya soka ukanda wa kusini kwa Amerika, ulichezwa katika mji wa Belo Horizonte-Brazil, na kushuhudia mabao ya wenyeji yakipachikwa wavuni na Philippe Coutinho, Neymar pamoja na Paulinho katika dakika za 25,45 na 59.

Ushindi huo kwa Brazil, unaiwezesha nchi hiyo kuendelea kuongoza msimamo wa kundi la kusini mwa Amerika kwa kufikisha point 24, zilizopatikana katika michezo 11 waliocheza mpaka sasa.

Argentina wamebaki katika nafasi ya sita kwenye msimamo huo kwa kuwa na point 16, hali ambayo inaendelea kuzusha hofu kwa taifa hilo kwenye harakati za kufuzu fainali za mwaka 2018.

Ukanda wa kusini mwa Amerika ya kusini hutoa washiriki watano wanaonaliza katika nafasi za juu kushiriki fainali za kombe la dunia, na taifa linalomaliza kwenye nafasi ya sita hucheza mchezo wa mtoano dhidi ya mshiriki kutoka ukanda wa Oceania kabla ya kujihakikishia nafasi ya kufuzu.

Michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia ukanda wa kusini mwa Amerika iliyochezwa leo alfajiri ni kwa saa za Afrika mashariki:

Uruguay 2 – 1 Ecuador

Paraguay 1 – 4 Peru

Venezuela 5 – 0 Bolivia

Colombia 0 – 0 Chile

Breaking News: Mbunge Hafidh Ali wa Jimbo la Dimani afariki dunia
Claudio Bravo Achafua Hali Ya Hewa Etihad Stadium