Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi usiku wa kuamkia leo aliwaongoza wenzake katika ushindi wa mabao matatu kwa sifuri waliouvuna mbele ya timu ya taifa ya Colombia, katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ukanda wa kusini mwa Amerika.

Messi alifunga bao la kuongoza kwa Argentina na kuongeza morari kwa wachezaji wenzake, kabla ya kupatikana kwa bao la pili ambalo lilifungwa na Lucas Pratto huku Angel Di Maria akifunga bao la tatu.

Ushindi huo umeiwezesha Argentina kufikisha point 19, ambazo zinawaweka katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa kundi la kusini kwa Amerika nyuma ya Ecuador na Chile.

Matokeo ya michezo mingine ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 ukanda wa kusini mwa Amerika.

Ecuador 3 – 0 Venezuela

Chile 3 – 1 Uruguay

Bolivia 1 – 0 Paraguay

Peru 0 – 2 Brazil

Matokeo ya michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia ukanda wa bara la Asia:

Kundi A

South Korea 2 – 1 Uzbekistan

China 0 – 0 Qatar

Syria 0 – 0 Iran

Kundi B

Japan 2 – 1 Saudi Arabia

Thailand 2 – 2 Australia

U.A.E. 2 – 0 Iraq

Kiwanda cha Konyagi, pombe kali feki chanaswa Dar
Gareth Southgate: Nimeleta Mabadiliko Kikosini