Mabingwa wa kombe la shirikisho Tanzania Bara (ASFC) Azam FC, huenda wakaendelea na michezo ya ligi kuu bila kocha mkuu Aristica Cioaba, ambaye bado yupo nchini kwao Romania.

Azam FC itarejea kwenye michezo ya ligi kuu ikiwa katika nafasi ya pili kwenya msimamo wa ligi kuu kwa kufikisha alama 54, nyuma ya vinara Simba SC wenye alama 71 huku Young Africans wakishika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 51.

Mkuu wa idara ya habari na mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria (Zaka Zakazi), amesema kuna uwezekano finyu kurejea kwa kocha wao mkuu wa Klabu hiyo Aristica Cioaba kutokana na mipaka ya nchi hiyo bado imefungwa kwa sababu ya janga la Corona.

Amesema ndege za kimataifa hazijaruhusiwa kuingia wala kutoka nchini Romania, hivyo huenda kocha huyo akashindwa kufika kwa wakati kwa ajili ya kukinoa kikosi chake kwenye maandalizi na kisha michezo ya ligi kuu na kombe la shirikisho.

Hata hivyo Zaka amesema baada ya kuona hivyo, uongozi wa Azam FC umefanya utaratibu wa kumrejesha haraka kocha wao msaidizi kutoka Burundi, Bahati Vivier kwa Private Car ambapo atafanya utaratibu wa kuvuka mpakani kule Kigoma.

Zaka amesema Vivier (kocha msaidizi) atakaimu ukocha mkuu huku kocha wa makipa Idd Abubakar atakuwa kocha msaidizi.

Pamoja na Serikali ya Tanzania kutangaza kurejea kwa ligi kuu Azam ndio Klabu pekee yenye wachezaji wengi wa kimataifa wako kwao jumla ya wachezaji 6 wapo nje ya nchi ambao ni: Nicholas Wadada (Uganda), Never Tegere, Donald Ngoma, Bruce Kangwa (Zimbabwe), Razak Abarola na Yakubu Mohamed (Ghana).

Wafahamu kidogo Ihefu Sports Club
Luc Eymael: Kikosi changu kitatisha

Comments

comments