Kocha Mkuu wa Feyenoord ya nchini Uholanzi Arme Slot amesema ataendelea kubakia klabuni hapo licha kuhusishwa na mpango wa kuwaniwa na Klabu ya Tottenham Hotspurs yenye maskani yake makuu jijini London.

Spurs walidhamiria kumnyakua kocha huyo baada ya kuiongoza klabu ya Feyenoord kushinda taji la Ligi Kuu ya Uholanzi msimu huu.

Imeelezwa kuwa Tottenham ilishindwa kuendelea na mpango huo baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kununua mkataba wa kocha huyo, Tottenham muda wote wamekuwa wakisisitiza kuwa hakuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Slot au Feyenoord na hawakutoa maoni yoyote hadharani kuhusu mwajiriwa huyo wa klabu nyingine.

Habari za ndani zinasema kwamba Slot alikuwa na kipengele kwenye mkataba wake kinachosema itaigharimu pauni milioni 5 kwa klabu inayomtaka kuvunja mkataba wa kocha huyo kwa Feyenoord.

Wakati ilipogundulika kuwa itaigharimu Spurs kiwango hicho cha fedha kinachofikia thamani ya pauni milioni 10 kama watataka kumuajiri Slot kwa sasa na pauni milioni tano nyingine kama watataka kuchukua na wasaidizi wake, viongozi wa Spurs waliamua kuondoka kwenye mazungumzo na kuwaeleza waendesha majadiliano hayo kuwa hawana uhitaji tena na kocha huyo.

Spurs imesema inadhani Slot ametumia ofa hiyo ya Spurs kupata mkataba mnono na klabu hiyo ya Uholanzi na sasa inafahamika wazi atasaini mkataba mpya na klabu ya Feyenoord.”

Ukitaka uzuri sharti udhurike - Wahenga
Iniesta amwaga machozi akiaga Vissel Kobe