Hatimaye Mlinda Mlango wa Dodoma Jiji FC Aron Kalambo amefunguka namna alivyopata wakati mgumu wa kuufuata mpira wa adhabu iliyopigwa na mshambuliaji mpya wa Young Africans Saido Ntibazonkiza, ambao ulizaa bao la pili kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumamosi (Desemba 19).

Kalambo amefunguka suala hilo kwa mara ya kwanza, hukuakikiria mkwaju uliopigwa na mshambuliaji huyo kutoka nchini Burundi ulikua mkali na ulistahili kuwa bao.

Kalambo amesema Ntibazonkiza aliupiga mpira ule kwa ufundi mkubwa, na yeye kama mlinda mlango alitumia uzoefu wake wote kujaribu kuuokoa,  lakinialishindwa na kujikuta nyavu zikitikisika.

Kalambo amesema ingawa anajua ana ubora wa kuzuia mipira ya adhabu, lakini kuna sehemu alizembea katika kufungwa bao hilo la pili katika mchezo huo, huku sehemu kubwa akimsifia Saido akidai alitumia akili na ufundi mkubwa kumuadabisha.

Kipa huyo wa zamani wa Taifa Stars, amesema wakati anaupanga ukuta wake katika adhabu hiyo alijua anayetaka kupiga ni mtu bora katika mipira ya adhabu, hivyo alijipa tahadhari akiupanga vyema ukuta wake, lakini akili nyingi za Saido zilimzidi ujanja.

“Mpigaji alikuwa fundi katika pigo lile, kwani hakutarajia kama angenitungua namna ile, kwa hakika huyu jamaa ana ujuzi mkubwa sana wa kupiga mipira ya adhabu.”

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Young Africans waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja, huku mabao mengine ya wakongwe hao katika soka la bongo yakifungwa na mabeki Lamine Moro na Bakari Mwamunyeto.

Bao pekee la Dodoma Jiji FC lilifungwa na mshambuliaji kutoka visiwani Zanzibar Abdallah Seif Karihe.

Mwambe: ibueni wawekezaji wapya wazawa
Maonyesho ya kilimo biashara kuwakutanisha wakulima zaidi ya 4,000