Klabu ya Everton imetangaza rasmi kumuweka sokoni mshambuliaji wake kutoka nchini Ubelgiji, Romelu Lukaku.

Everton wametangaza kiasi cha Pauni milion 75 kama ada sahihi ya mshambuliaji huyo ambaye anawaniwa na klabu kadhaa za ndani na nje ya nchini England.

Klabu ya Arsenal na Chelsea zote za nchini England zimetajwa kuwa katika mipango ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo huku klabu bingwa nchini Italia Juventus ikiwa sehemu ya mpururo huo pamoja na Real Madrid ya Hispania.

Arsenal ambao tayari wameshamkosa mshambuliaji wa klabu bingwa nchini England, Leicester City,  Jamie Vardy wanatajwa kuwa mstari wa mbele katika harakati za kumuwania Lukaku, lakini kwa upande wa Chelsea nguvu za ziada zinaripotiwa kufanywa ili kufanikisha hatua za kumrejesha mshambuliaji huyo.

Chelsea wanahitajia kukamilisha mpango wa kumrejesha Lukaku kwa kutaka kutengeneza ushirikiano mzuri katika safu yao ya ushambuliaji, baada ya kumsajili Michy Batshuayi kwa ada ya uhamisho wa paund milion 33.

Wawili hao wanatajwa kuwa na uhusuano mzuri wanapocheza pamoja, wakiwa na timu yao ya taifa ya Ubelgiji ambayo mwishoni mwa juma lililopita iliambulia kisago cha kufungwa mabao matatu kwa moja dhidi ya Wales na kutupwa nje ya michuano ya Euro 2016 huko Ufaransa.

Joseph Omog Awaita Wachezaji Wote Mazoezini
The Eagles Wajipanga Upya Kwa Christian Benteke Liolo