Washindi Wa Ngao Wa Jamii Nchini England Arsenal FC, wameripotiwa kutuma ofa ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini brazil na klabu ya PSG Lucas Rodrigues Moura da Silva.

Tovuti ya UOL Esporte ya nchini Brazil imeandika kuwa, mchezaji huyo ameonyesha kuwa tayari kuondoka jijini Paris, kutokana na mazingira ya mji huo kumchosha.

Arsenal kupitia kwa meneja wao Arsene Wenger wameripotiwa kutuma ofa ya pauni milioni 27, ambazo ni sawa na Euro milioni 30.

Wenger ameuthibitishia uongozi wa Arsenal kumuhitaji mchezaji huyo katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa 2017/18, na anaamini atamsaidia katika harakati za kusaka taji la PL ambalo hajawahi kulichukua kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Hata hivyo Lucas ametangaza msimamo kwa klabu yoyote itakayokua tayari kumn’goa jijini Paris, kwa kuitaka imuandalie mkataba ambao utamuwezesha kucheza katika kikosi cha kwanza.

Lucas tayari ameshaitumikia PSG katika michezo 145 na kufunga mabao 32 tangu alipotua klabuni hapo mwaka 2013 akitokea Sao Paulo.

Mzee wa Upako amvutia Q-chief
Kiongozi msaidizi wa Samsung mbaroni kwa ufisadi