Klabu ya Arsenal imethibitisha kumsajili kiungo kutoka nchini Uswiz, Granit Xhaka akitokea Ujerumani alipokua akiitumikia klabu ya Borussia Monchengladbach kwa ada iliyofanywa kuwa siri.

Taarifa iliyowekwa katika tovuti ya klabu ya Arsenal imethibitisha kusajili kwa Granit Xhaka mwenye umri wa miaka 23 kwa makubaliano ya mkataba wa muda mrefu.

Pamoja na makubaliano ya pande hizo mbili ya ada ya usajili wa mchezaji huyo kufanaya siri, upekuzi wa baadhi ya vyombo vya habari vya nchini England umebaini kwamba, Arsenal wametoa kiasi cha Pauni milioni 30.

“Granit Xhaka ni mchezaji mwenye vigezo vya kuitumiki Arsenal, na amekuwa na shauku ya kucheza michuano mikubwa kama ligi ya mabingwa barani Ulaya, nina uhakika hapa atakamilisha jambo hilo, kwa mafanikio makubwa” Alisema meneja wa Arsenal, Arsene Wenger kuputia tovuti ya klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

“Tulimfuatilia kwa muda mrefu na tulitambua ana kipaji cha kucheza soka. Na baada ya kukamilisha usajili wake tunamtakia kila la kheri Granit katika maandalizi yake kuelekea fainali za Euro 2016 sambamba na timu yake ya taifa ya Uswiz.” Aliongezea Wenger

Arsenal wameanza na usajili wa Xhaka, ikiwa ni sehemu ya kuziba mapengo yaliyoachwa wazi na wachezaji waliokua wanacheza nafasi ya kiungo Tomas Rosicky, Mikel Arteta pamoja na Mathieu Flamini ambao wote kwa pamoja na walitangaza kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

Xhaka, mejiunga na Arsenal huku akiacha historia ya kucheza michezo 102 katika ligi ya nchini Ujerumani na kwa upande wa timu yake ya taifa ya Uswiz ameichezea michezo 41.

Video: Mjusi wa Tanzania Aliyepelekwa Ujerumani Atua Bungeni, Mbunge Afichua Haya
Rafael Benitez Akubali Kubaki Newcastle United