Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza suala la ushindi katika mchezo wa hii leo ambapo kikosi chake kitakua nyumbani kikipambana dhidi ya mabingwa wa soka kutoka nchini Ugiriki, Olympiakos.

Wenger amesisitiza jambo hilo kikosini mwake, kutokana na mambo kuwaendea vibaya katika mchezo wa kwanza kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kupitia kundi F, ambapo The Gunners walikubali kupoteza kwa kufungwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Dynamo Zagreb majuma mawili yaliyopita.

Wenger amesema mchezo wa hii leo una umuhimu mkubwa sana katika kikosi chake, kutokana na hitaji la point tatu muhimu katika msimamo wa kundi F, na anaamini maandalizi aliyoyafanya kuelekea katika mtanange huo yatatosha kufikia lengo walilo likusudia.

Amesema ni wakati mzuri kwa kila mmoja kikosini mwake kwa kuamini yaliyofanyika katika mchezo wa kwanza wa kundi F, yalitokana na bahati mbaya, na hii leo ni wakati mzuri kuonyesha wapo tayari kurekebisha makossa yao.

Katika mchezo wa kwanza wa kundi F, Arsenal walimaliza pungufu baada ya mshambuliji wao kutoka nchini Ufaransa, Olivier Giroud kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia mchezo wa hovyo aliouonyesha katika kipindi cha pili.

Marco Silva: Nitavunja Mwiko Wa Kufungwa England
Msingwa Na Wafuasi Wa Chadema Watupwa ‘Selo’