Klabu ya Arsenal ya nchini Uingereza ipo mbioni kukamilisha dili la kumsajili Mshambuliaji wa klabu ya Lille ya nchini Ufaransa,Nicolas Pepe.

Klabu zote mbili zimefikia makubaliano kwaajili ya kumsajili winga huyo raia wa Ivory Cost kwa ada ya £72M.

Aidha, mazungumzo kati ya Arsenal na wawakilishi wa Pepe yanaendelea na Arsenal wana uhakika wa kukamilisha dili hilo masaa machache baadae.

Inasemekana kuwa Arsenal watalipa pesa hizo kwa awamu katika mkataba wa miaka mitano yote.

Klabu kadhaa zimekuwa zikimfukuzia winga huyo zikiwemo klabu ya Napoli, Liverpool na Manchester United lakini klabu ya Arsenal ndiyo imekuwa na uhakika wa kuinasa saini ya mchezaji huyo.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 29, 2019
Ujumbe wa IGP Sirro kuhusu mali za askari

Comments

comments